Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama liko Nairobi kujadili hali ya Somalia

Baraza la usalama liko Nairobi kujadili hali ya Somalia

Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa umeanza leo mjini Nairobi Kenya kujadili mgogoro wa Somalia.

Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo ni ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga, serikali ya mpito ya Somalia, wadau muhimu wa kisiasa ikiwemo Rais wa jimbo lililojitenga la Puntland na Galmadug na wawakilishi wa jumuiya za kijamii za Somalia.

Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi anafuatilia mkutano huo na hii hapa taarifa yake.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)