Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawarejesha Haiti watoto waliosafirishwa kiharamu Jamhuri ya Dominican

IOM yawarejesha Haiti watoto waliosafirishwa kiharamu Jamhuri ya Dominican

Shirika la umoja wa mataifa linlohusika na uhamiaji IOM linawasafirisha makundi ya watoto ambao walipelekwa nchini Dominica kwa ajili ya kutumikishwa kwenye kazi mbalimbali ambapo sasa watoto hao wanasindikizwa hadi kwa familia zao nchini Haiti.

Katika hatua ya kwanza kundi la watoto 8 tayari limesafirishwa kuelekea nyumbani  chini ya ushirikiano wa mamlaka za ulinzi wa watoto wa pande zote mbili.

Hata hivyo hili ni kundi la pili katika mfululizo wa mpango wa kuwarejesha watoto hao nyumbani na kuwaunganisha na familia zao baada ya kusafirishwa kiharamu hadi katika nchi hiyo ya Dominica.

Serikali ya Dominica hivi karibuni iligundua kuwepo kwa kundi kubwa la watoto waliosafirishwa nchini humo kwa njia ya magendo kwa ajili ya kutumikishwa kwenye kazi mbalimbali.