Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kulipuka kwa Volkano nchi Iceland kuazua utata:

Kulipuka kwa Volkano nchi Iceland kuazua utata:

Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO linasema kuwa ripoti zinaeleza kuendelea kulipuka kwa volkano nchini Iceland. WMO inasema kuwa kuwepo kwa majivu kutoka kwa mlima huo kutategema na muda ambao mlima utachukua kuvuja na hali ya hewa.

Hata hivyo kituo cha utafiti wa masuala ya volkano mjini London kitaendelea na utabiri wake wa masaa 24 ili kusaidia katika kutoa maamuzi. Ujumbe huu unatolewa kwa idara za kusimamia safari za ndege, viwanja vya ndege, na mashirika ya ndege ili waweze kufanya uamuzi iwapo ndege inaweza kufanya safari kwa njia salama kulingana na vile Claire Nulis kutoka WHO anavyoeleza.

(SAUTI YA CLAIRE NULIS)