Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Helkopta za UNMIS zashambuliwa Abyei

Helkopta za UNMIS zashambuliwa Abyei

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMIS umearifu kwamba leo jioni saa za Sudan helkopta zake nne ambazo zilipaa salama zimeshambuliwa .

Kwa mujibu wa UNMIS raundi 14 za mashambulizi ya risasi zimefanyika kutoka kila pambe karibu na ofisi za mpango huo.

Helkopta hizo ambazo zikuwa na marubani tuu ndani zilikwepa mashambulizi yote na kufanikiwa kutua salama WAU uwanja wa ndege wa Western Bar El Ghaza ambao uko kwenye ofisi ya pili ya UNMIS.

UNMIS inasema hali bado ya wasiwasi Abyei na mpango wa Umoja wa Mataifa utaendelea kufuatilia kwa karibu inavyoendelea.