Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji kwenye mpaka wa Chad wanahitaji msadaa:IOM

Wahamiaji kwenye mpaka wa Chad wanahitaji msadaa:IOM

Kundi kutoka shirika la kimataifa la uhamaiaji IOM lililotumwa kuchunguza hali ya wahamaiji wanaokimbia ghasia nchini Libya na kuingia nchini Chad linasema kuwa maji, chakula na huduma za kiafya ni kati  ya vitu vinavyohitajka kwa dharura.

Hata kama wahamiaji 3800 ambao waliripotiwa kukwama kwenye kijiji cha Zouarké kwa wiki kadha wamefanikiwa kujihudumia, wafanyikazi wa IOM katika eneo hilo wanasema kuwa wahamiaji 1200 huwa wanawasili kwa wakati mmoja wakiwemo wanawake na watoto. Kwa sasa kijiji hicho kimelemewa na idadi hiyo katika huduma za maji huku wakitegemea kisima kimoja tu. Jumbe Omari Jumbe anaeleza

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)