Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya UM ataka kuzitishwa kwa ghasia mjini Abyei:

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya UM ataka kuzitishwa kwa ghasia mjini Abyei:

Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu watu 20,000 wamekimbia mji ulio Sudan Kusini wa Abyei baada ya wanajeshi kutoka jeshi la Sudan kulidhibiti eneo hilo linalozozaniwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu linasema idadi ya waliokimbia makwao huenda ikaongezeka kwa kuwa mashirika ya kutoa misaada hayakuweza kufika maeneo yaliyoathirika kutokana na sababu za kiusalama.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pilaaay anataka kusitishwa kwa ukatili unaoendelea na kuongeza kuwa mzozo kati ya wanajeshi wa Sudan na wale SPLM kutoka kusini ni kizingiti kwa amani kati ya Kusini na Kaskazini. Rupert Colville ni kutoka afisi ya tume ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)