Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban njiani kuelekea Ethiopia akitokea Nigeria

Ban njiani kuelekea Ethiopia akitokea Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwa sasa yuko safarini kuelekea nchini Ethiopia baada ya kukamilisha ziara yake nchini Nigera katika jitihada za kuunga mkono mradi wa kuwahakikishia afya bora akina mama na watoto aliouzindua mwaka uliopita wakati wa mkutano wa malengo ya milenia.

Kabla ya kuondoka nchini Nigeria Ban alihutubia mkutano wa magavana na kuelezea kuhusunishwa na ghasia zilizotokea nchini humo hasa kwenye majimbo ya kaskazini kufuatia uchaguzi wa urais wa hivi majuzi. Pia Ban alielezea hisia zake kuhusiana na ghasia za kikabila na kidini zinazotokea mara kwa mara nchi humo akiongeza kuwa magavana ndio wanastahili kuwa kwenye mstari wa mbele katika kutatua matatizo haya. Ban amewataka kuhakikisha kuwa kuna usawa katika utoaji wa huduma za afya na pia kuhakikisha kuwa ufadhili kwa huduma za afya kwa akina mama na watoto unapatikana na kutolewa kwa njia inayofaa kote nchini.