Ban akutana na Rais wa Nigeria mjini Abuja

Ban akutana na Rais wa Nigeria mjini Abuja

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon alikutana asubuhii hii na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan mjini Abuja. Walizungumzia ushirikiano kati ya Umoja wa mataifa na Nigeria nchi ambayo imekuwa inaongoza na kuchangia kuwepo na utulivu na maendeleo katika eneo la Afrika ya Magharibi.

Katibu mkuu amempongeza Rais wa Nigeria kuhusu mchango wake wa kumaliza mzozo wa Cote D’ Ivoire. Katibu mkuu Ban na rais Jonathan walizungumzia pia swala la kutenguka usalama katika Sudan Kusini na jinsi ya kusaidia kufikia uhuru wa Sudan kusini baadae mwezi julai.

Wamejadili pia umuhimu wa kuwepo na uelewa wa pamoja kuhusu mzozo wa Lybia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepongeza serikali ya Nigeria baada ya bunge kuidhinisha mswada wa sheria ya afya utaosaidia kupangilia bajeti ya huduma za afya muhimu nchini Nigeria. Alisema kwamba matumaini yake ni kuona mataifa mengine yanaiga mfano huo.

Viongozi hao walijadili pia ushirikiano katika vita dhidi ua ugaidi na juhudi za kupamba na utapakaji wa silaha ndogondogo.