Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto za uchumi unaojali mazingira kujadiliwa:UNESCO

Changamoto za uchumi unaojali mazingira kujadiliwa:UNESCO

Kongamano la kimataiafa ambalo linashabaya ya kujadilia mustakabala wa dunia na mazingira yake linafanyika kesho mji Paris huku wajumbe wakitazamiwa kutuwama kwenye mada zinazohusu changamoto juu ya kufikia uchumi unaojali mazingira pamoja na jamii ambayo pia inayojali mazingira hayo.

Kongamano hilo ambalo linafanyika kwenye makao makuu ya shirika la umoja wa mataifa linalohusika na sayansi, elimu na utamaduni UNESCO, ni sehumu ya maandalizi kuelekea kwenye mkutano wa kimataifa wa mazingira endelevu utakaofanyika Rio de Janeiro, Brazil, mwaka  2012.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova pamoja na Katibu Mtendaji wa kamishna ya umoja wa mataifa kwa nchi za ulaya Ján Kubiš,watazindua kongamano hilo.

Ama wajumbe wengine ambao wanatazamiwa kuhudhuria kongamano hilo ni pamoja na Michel Rocard, ambaye ni rais mwenza wa taasisi ya Collegium na pia waziri mkuu wa zamani wa ufaransa na Rais wa Jamhuri ya Slovenia Danilo Türk.