Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM utaisaidia Ivory Coast kurejea maisha ya kawaida:Ban

UM utaisaidia Ivory Coast kurejea maisha ya kawaida:Ban

Kwa mara ya kwanza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana na wahanga wa matukio vurugu za kisiasa nchini Ivory Cost na kuelezea namna anavyowahuzunikia kutokana na kadhia zinazowakumba, lakini amehaidi kuendeleza kuunga mkono harakati za kulijenga upya taifa hilo.

Akiwa kwenye mji mkuu wa Abidjan, Ban amehaidi kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwa bega kwa bega na wananchi hao ambao wameanza kuchukua nira mpya ya kulijenga taifa hilo na kurejesha sura ya umoja wa kitaifa.

Ban aliwaambia wananchi hao ambao sasa wanaitazamwa kama wakimbizi wa ndani kuwa “ nataka mtambue kuwa moyo wangu upo pamoja nanyi, kwa maana hiyo ndiyo maana leo hii nipo hapa ili kuonyesha mshikamano wangu, na pia kuweza kutoa msaada wa hali na mali ili hatimaye maisha yenu yarejea kwenye hali ya kawaida”.

Ameiahidi kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea na utoaji wa misaada ya kibinadamu ikiwemo usambazaji wa mahitaji muhimu kama maji, chakula,maskani pamoja na huduma za kiafya.