Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMIS yaalani uporaji na machafuko Abyei

UNMIS yaalani uporaji na machafuko Abyei

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan umelaani vikali uporaji unaondeshwa na makundi yaliyojihami kwenye mji wa Abyei nchini Sudan ukisema kuwa vikosi vya Sudan ndivyo vilivyo na jukumu la kulinda maeneo vinaoyadhibiti.

Ujumbe huo unatoa wito kwa seikali ya Sudan kwa haraka kuhakikisha vikosi vya Sudan vitatimiza wajibu wao na kuingilia kati kukomesha vitendo hivyo vya kihuni.

(SAUTI YA KOUIDER ZERROUK-UNMIS)

Nalo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linasema kuwa hatua za wanajeshi wa Sudan za kuchukua udhibiti wa eneo la Abyei ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya amani ya CPA.

Mkataba huo uliotiwa sahihi mwaka 2005 ulimaliza mapigano ya miongo miwili ya wenyewe kwa wenyewe kati ya eneo la kaskazini na kusini mwa nchi. Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema kuwa anasumbuliwa na hali ya usalama ya raia katika eneo hilo.