Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zatakiwa kuwekeza kuzuia magonjwa sugu:WHO

Serikali zatakiwa kuwekeza kuzuia magonjwa sugu:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa kutokana na gharama kubwa ya kuyatibu mgonjwa sugu kama vile ugonjwa wa saratani , kisukari pamoja na magonjwa ya moyo na ya kupumua watu zaidi kwenye kwenye nchi zinazoendelea wanazidi kujipata kwenye umaskini.

Huku watu milioni 36 wakifa kila mwaka kutokana na magonjwa hayo WHO inatoa wito kwa serikali kutenga fedha zaidi katika programu za kuzuia magonjwa haya.

Kati ya masuala yanayochangia kuwepo kwa magonjwa haya ni pamoja na uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe , kutokula vyakula vyenye afya pamoja na kutofanya mazoezi ya kimwili.

Dr Ala Alwan kutoka WHO anasema kuwa kwa kujizuia na tabia kama hizi karibu maisha milioni tisa yanaweza kuokolewa kila mwaka kote duniani.

(SAUTI YA DR ALA ALWAN)