Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Boti ya IOM iliyosheheni wahamiaji yaelekea Benghazi

Boti ya IOM iliyosheheni wahamiaji yaelekea Benghazi

 

Boti ya IOM ikiondoka MisrataMashua ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM inayowasafirisha wahamiaji 600 pamoja na raia wengine waliojeruhiwa kutoka mji wa Misrata inatarajiwa kuwasili kwenye mji wa mashariki mwa Libya wa Benghazi baadaye hii leo.

Shughuli hiyo ambayo ni ya saba kuendeshwa na IOM tangu mwezi Aprili ilikuwa na lengo la kuwakoa wahamiaji waliokwama kwenye mji wa Misrata tangu kuanza kwa mzozo nchini Libya mwezi Februari. Waliookolewa ni pamoja na raia 392.

Ilipowasili mjini Misrata mashua hiyo ilikuwa imesheheni chakula cha msaada zikiwemo tani 150 za unga wa ngano pamoja na tani 130 za mboga na bidhaa zingine vikiwemo pia vifaa vya kutoa matibabu. Jumbe Omari Jumbe afisa wa IOM anafafanua

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)