Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misitu ni nguzo ya kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa:FAO

Misitu ni nguzo ya kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa:FAO

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na Benki ya Dunia wameanzisha mpango mwongozo mpya ambao utasaidia nchi kukadiria usimamizi wa misitu yao.

Mwongozo huo unazipa nchi hizo njia ya kukagua , kutambua na kusuluhisha matatizo yanayokumba usimamizi wa misitu.

Pia mwongozo huo utahakikisha kuwa jitihada za kupunguza gesi chafu kutoka kwa misitu kwenye nchi zinazondelea zinasimamiwa kwa njia mwafaka . Flora Nducha anaripoti.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)