Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi katika masuala ya kijamii utasaidia kumaliza umasikini

Ulinzi katika masuala ya kijamii utasaidia kumaliza umasikini

Serikali za mataifa ya Asia na Pacific zinazohudhuria mkutano wa maendeleo mjini Bangkok zimekubalina kuwepo kwa ulinzi katika masuala ya kijamii kama moja ya njia ya kuwaondoa kwenye uamskini na kutengwa kwa mamilioni ya watu wao.

Kulingana na utafiti wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kichumi, kijamii kwa nchi za Asia na Pacific UN –ESCAP ulio ajenda kuu ya mkutano wa tume hiyo unaoendelea mjini Bangkok unasema kuwa ulinzi katika masuala ya kijamii una manufaa katika masuala ya kiuchumi.