Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Ivory Coast waanza kupata tena matumaini ya maisha

Watoto Ivory Coast waanza kupata tena matumaini ya maisha

Zaidi ya raia 500,000 wa Ivory Cost wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameripotiwa kukuimbia nchini humo kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyosababishwa na matokeo ya urais wa mwezi Novemba .

Hata hivyo hali ilikuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita ambako zaidi ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni moja walikosa makazi yao kutokana na mvutano mkali wa kisasa uliharibu kabisa sura ya nchi hiyo.

Ripoti zinasema kuwa kwa hivi sasa kumeanza kuchomoza sura mpya ya matumaini ambapo watu wameanza kujenga maaminiano lakini hata hivyo kundi kubwa la watu bado wapo kwenye kihoro kikubwa.

Tayari shirika la umoja wa mataifa linalohusika na watoto UNICEF limeanzisha kituo maalumu kwa ajili ya utoaji wa msaada wa kisaikolojia na makuzi mapya kwa watoto ambao bado wanasumbuliwa na jinamizi la machafuko hayo.