Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kutoa semina ya mikopo Sri Lanka

IOM kutoa semina ya mikopo Sri Lanka

Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, litaaendesha maonyesho ya siku mbili nchini Sri Lank maonyesho ambayo yanakusudia kuwapa uwezo wa kiuchumi jamii ya wahamiaji walioko nchini humo.

Maonyesho hayo yanayofahamika kama “Credit Fair” yanafanyika mwishoni mwa juma katika mji wa Ampara ulioko mashariki kwa Sri Lank na yanatazamiwa kuwafaidia jumla ya washiriki 4,000.

Taasisi kadhaa za kifedha nazo zimealikwa kwenye maonyesho hayo ambayo yatashiriki kutoa elimu juu ya mikopo.

Eeneo hilo la Ampara linatajwa kuwa na taasisi kadhaa za kifedha ambazo hutoa mikopo kwa wananchi, lakini ni wakazi wachache wa eneo hilo wenye ufahamu sahihi juu ya ukopaji na matumizi yake.