Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirika wa silaha Colombia kulipwa fidia

Waathirika wa silaha Colombia kulipwa fidia

 

Makundi kadhaa ya watu walioathiriwa na matumizi haramu ya silaha nchini Colombia yameanza kuwasilisha mpango ambao unataka ulipwaji fidia kwa wahanga wa mateso hayo.

Mpango huo tayari umewasilishwa kwa serikali za kijimbo. Ikifanya kazi pamoja na kamishna ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya utoaji fidia ,shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji IOM imezibainisha jamii za makundi sita ambazo zimeanzishwa kama mpango wa majaribio ili kufikia shabaya ya ulipwaji wa fidia hiyo.

Kwa mujibu wa afisa wa IOM, hatua ya kuanzisha mpango wa utoaji fidia, ni kitendo cha kihistoria ambacho hakijapatwa kufanywa sehemu nyingine yoyote isipokuwa sasa nchini Colombia.