Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa haki za binadamu akamilisha ziara Burundi

Mtaalamu wa haki za binadamu akamilisha ziara Burundi

Mtaalamu huru wa umoja wa mataifa kuhusu haki za binaadamu Burundi amekamilisha ziara ya siku nne nchini humo .

Fatsah Ougergouz amesema pamoja na Burundi kupiga hatua katika kuimarisha haki za binaadamu ,lakini bado mengi ya kufanywa hasa kumaliza mauji dhidi ya raia yanayoendeswa katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Mtaalau huyo atawasilisha ripoti yake katika Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binaadamu baadae mwezi juni. Kutoka Bujumbura ,Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA anatuarifu zaidi.