Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 16 zaahidi kuunga mkono UM katika kupunguza vifo vya uzazi

Nchi 16 zaahidi kuunga mkono UM katika kupunguza vifo vya uzazi

Jumla ya nchi 16 zimetangaza ahadi ya kujitolea katika kupunguza vifo vya uzazi, vya watoto wakati wa kuzaliwa na vya watoto wachanga. Ahadi hizo zinafikisha idadi ya nchi zilizojitolea kuwa 34 , 27 kati yao kutoka barani Afrika.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo hilo akisema kuwa kujitolea huku kunatoa msukumo mpya katika kutatua matatizo ya kiafya yanayowakumba wanawake na watoto.

Kujitolea huku kunakoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS , Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF , Benki ya Dunia na shirika la afya duniani kunaangazia hatua za kupunguza vifo , kuzuia maamubuzi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na chanjo dhidi ya watoto.