Israel na Palestina zashauriwa kufanya juhudi mpya za amani

20 Mei 2011

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi nchini Israel na kwenye utawala wa Palestina kuwa na matumaini mapya ya kuwepo kwa mataifa mawili katika kumaliza mzozo ya Israel na Palestina.

Akijibu hotuba ya rais wa Marekani Barack Obama aliyoitoa siku ya Alhamisi Ban amesema kuwa rais Obama ametoa maoni muhimu yanayoweza kusaidia kusonga mbele kwa mazungumzo ya amani.

Kwenye hotuba yake rais Obama alisema kuwa mpaka kati ya Isrel na Palestina unastahili kufuata ramani ya mwaka 1967 akiongeza kuwa mipaka iliyo salama na inayotambulika inastahili kubuniwa kwa pande zote mbili. Ban amesema kuwa kuna matumaini ya kupatikana kwa makubalino ya amani yanayoruhusu mataifa mawili tofauti kukaa pamoja kwa amani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter