Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la Ugonjwa wa saratani laongezeka duniani: WHO

Tatizo la Ugonjwa wa saratani laongezeka duniani: WHO

 

Huku shirika la kimataifa linaloendesha utafiti kuhusu ugonjwa wa saratani likitarajiwa kujapisha makala kuhusu ugonjwa wa saratani kundi moja kwa sasa linakutana kubaini ikiwa kuna uhusiano wowote kati ya ugonjwa wa saratani na matumizi ya Radio , Runinga au simu za mkononi. Matokeo ya utafiti huo yanatarajiwa kutangazwa mjini Lyon mwishoni mwa mwezi Mei. Inaripotiwa kuwa visa vya ugonjwa wa saratani vinaongezeka huku visa milioni 12 vikiripotiwa mwaka 2008. Kituoa cha utafiti wa ugonjwa huo kinakadiria kuwa visa vya ugonjwa wa saratani vitapanda hadi visa milioni 27 ifikapo mwaka 2030. Dr Nicolas Gaudin kutoka shirika la afya duniani WHO anaeleza.

(SAUTI YA DR NICOLAS GAUDIN)