Ingawa imepiga hatua Burundi bado ina changamoto katika vita vya ukimwi

20 Mei 2011

Lengo namba sita ni kupambana na ukimwi, malaria na maradhi mengine. Na leo hii tunajikita katika kukabiliana na ukiwmi. Viongozi nchini Burundi ,Viongozi wanasema juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi zinaonekana kupiga hatua .

Taakwimu za karibuni zinaonyesha kwamba maambukizi yamepungua sana hasa katika maeneo ya mijini ambako awali idadi ya maambukizi ilikuwa kubwa sana.

Umoja wa Mataifa na mashirika yake likiwemo la ukimwi UNAIDS, la afya WHO, la watoto UNICEF, la idadi ya watu UNFPA na wanaharakati wengine wamekuwa wakipiga debe kuzichagiza serikali kufanya kila liwezekanalo japo kupunguza kwa asilimia 50 ya tatizo hilo hapo 2015.

Japo kuna nchi zimepiga hatua kuna zingine kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, bado zinasuasua. Kwa upande wake Burundi inasema imejitahidi kwani sasa inaorodhesha watu laki mbili unusu tu wenye virusi vya ukimwi sawa na asilimia 4 ya wakaazi wote wa Burundi , lakini bado inaghubikwa na changamoto na kubwa ni kudhibiti maambukizi katika maeneo ya vijijini ambako kumekuwa na taarifa za maambukizi mapya.

Tatizo lingine kubwa ni uhaba wa dawa za kufubaza makali ya viruzi vya ukimwzi au ARV’s ambazo mara kwa mara hukosekana , na serikali na mashirika ya kuwasaidia waathirika wamekuwa wakisontwa kidole kwa kufuja msaada wa fedha toka kwa wafadhili na hivyo kutoa tisho kubwa kwa wafadhili kutaka kukatisha misaada hiyo.

Ikiwa imesalia miaka mine tuu kabla ya 2015 ambapo viongozi wa dunia walikubaliana kuwa muda wa kutimiza lengo hili na mengine saba, je Burundi itafika? Mwandishi wetu wa Bujumbura wetu Ramadhani KIBUGA anatanabahi katika makala hii ,Ungana naye.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter