Mfuko wa UM wa kuokoa maisha wapindukia dola bilioni 2

19 Mei 2011

 

Zaidi ya dola bilioni mbili zimetolewa na mfuko wa Umoja wa mataifa wa dharura CERF kusaidia katika matatizo mbalimbali yaliyiosababishwa na majanga ya asili na vita.

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema hizi ni juhudi kubwa za kuharakisha kukabiliana na matatizo ya kibinadamu duniani.

Mfuko wa CERF unapata mchango wa fedha kutoka katika serikali, mashirika , watu binafsi, wahisani na mashirika yasiyo ya kiserikali. Martin Nesirky ni msemaji wa Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA MARTIN NESIRKY)

Mfuko huo wa msaada ulizinduliwa mwaka 2006 na umekuwa ni chanzo cha sita cha mapato ya Umoja wa mataifa kwa msaada wa kibinadamu, ukitoa fungu la wastani wa dola milioni 400 kwa mwaka kwa nchi 82.

Katibu Mkuu amesema nchi wanachama walianzisha CERF kwa kwababu rahisi, wakati watu wakikumbwa na majanga hakuna muda wa kupoteza. CERF imethibitisha kuwa mkombozi wa maisha.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter