Tuzo 6 za UM zatolewa kwa kukabilia majanga

Tuzo 6 za UM zatolewa kwa kukabilia majanga

Shirika linalohusika na kupambana na uchafuzi hatari wa mazingira kwenye nchi zinazoendelea na msomi mmoja anayeshughulika kuhakikisha usalama wa nyumba wakati wa mitetemeko ya ardhi ni kati ya waliopokea tuzo kutoka kwa Umoja wa Mataifa na kundi moja la kimazingira.

Tuzo jingine liliiendea taasisi ya Blacksmith kwa kujitolea kwake katika kusuluhisha matatizo ya uchafuzi wa mazingira kwenye nchi maskini na zilizo na kipato cha wastani ambapo afya ya binadamu iko kwenye hatari.

Wengine ni Dionysia-Theodora mwanasheria raia wa Ugiriki aliyetuzwa kwa jitihada zake za kuunga mkono ujenzi mpya baada ya majanga ya kiasili kama vile janga la moto uliotekekeza sehemu ya eneo la Peloponnese nchini Ugiriki mwaka 2007.