Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unasiaida maafisa wa afya Uganda baada ya homa ya Ebola

UM unasiaida maafisa wa afya Uganda baada ya homa ya Ebola

Shirika la afya duniani WHO linausaidia uongozi wa Uganda kuchunguza kisa cha homa ya Ebola ambacho kimekatili maisha ya msichana wa miaka 12 katika taifa hilo la Afrika ya Mashariki mapema mwezi huu.

Msichana huyo kutoka wilaya ya Lowero katikati mwa Uganda alikufa saa chache baada ya kulazwa hospitali Mai 6 lakini alikuwa mgonjwa kwa siku tano.

Kwa mujibu wa WHO chunguzi wa maabara mjini Entebbe umethibitisha kuwepo kwa virusi vya Ebola ikiongeza kwamba sasa vipimo vimepelekwa kwenye kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa CDC kilichopo Atlanta hapa Marekani kwa uchunguzi zaidi.Uganda ilishawahi kukabiliwa na lipuko wa homa ya Ebola na 2008 serikali ilitangaza mlipuko huo wa karibuni umetokomezwa. Mgonjwa wa Ebola anakuwa na dalili za homa kali, kudhoofika, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa, kuwashwa kooni, kutapika, kuhara, kutokwa vipele na matatizo ya figo na ini.