Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafiriwa wafanyakazi wa misaada wasitishwa Darfur kwa ajili ya usalama

Usafiriwa wafanyakazi wa misaada wasitishwa Darfur kwa ajili ya usalama

Umoja wa Mataifa unasema kuwa utawala nchini Sudan umetangaza kupiga marufuku kusafiri kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za kibinadamu wanaohudumu kusini mwa jimbo linalokumbwa na mzozo la Darfur kutokana na oparesheni za kijeshi zinazoendelea pamoja na ukosefu wa usalama.

Kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na cha Mungano wa Afrika cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur UNAMID kinasema kuwa tume ya kutoa huduma za kibinadamu nchini Sudan ilikiarifu kikosi hicho yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuwa usafiri umepigwa marufuku.

Tangazo hili linajiri siku mbili baada ya wanajeshi wa Sudan kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya mji ulio kusini mwa Darfur wa Labado na kijiji cha Esheraya.