Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa UM kuzuru Australia

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa UM kuzuru Australia

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay wiki hii ataanza ziara Ijumaa wiki hii nchini Australia kujadili masauala ya haki za binadamu.

Pillay atakutana na viongozi wa serikali, tume ya haki za binadamu ya Australia, jamii za watu wa asili wa Aboriginal na Torres Strait na maashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika siku sita za ziara hiyo Bi Pillay pia atazuru miji ya Darwin, Cairns, Sydney na Canbera. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)