Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufisadi umekithiri Magharibi mwa Balkans:UNODC

Ufisadi umekithiri Magharibi mwa Balkans:UNODC

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na uhalifu UNODC linasema kuwa mmoja kwa kila ya watu sita kwenye eneo la magharibi mwa Balkans walipitia aina fulani ya ufisidai kutoka kwa afisa wa serikali katika kipindi cha mwaka uliopita.

Kulingana na ripoti ya shirika hilo ambapo watu 28,000 walihojiwa kwa ufadhili wa tume ya ulaya ilionyesha kuwa tatizo la ufisadi limechukua nafasi ya tatu kati ya masuala yanawasumbua wenyeji wa eneo hilo baada ya ajira na umaskini.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa ufisadi ni suala la kila siku huku wanaopokea hongo wakiwa ni pamoja na madaktari , maafisa wa polisi , wauguzi na maafisa wa manispaa.