Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa hali ya hewa wakutana Geneva

Wataalamu wa hali ya hewa wakutana Geneva

Zaidi ya wataalamu wapatao 600 wanakutana huko Geneva kwa ajili ya mkutano wa umoja wa mataifa ambao unajadilia suala la hali ya hewa.

Wajumbe hao kwenye mkutano huo ambao utadumu kwa muda wa wiki tatu, wanatazamia kubainisha mipango ambayo itazisaidia nchi mbalimbali kuchukua mkondo mpya wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huo unatazamiwa kuweka sera mpya kwa ajili ya kuisamilisha dunia na majanga ya kimaumbele yanayoweza kujitokeza katika siku za usoni.

Katika ujumbe wake uliotolewa kwenye kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moo amehimiza umuhimu wa kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuzitatua kirahisi changamoto zinazoendelea kuikabili dunia hivi sasa.