Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kimataifa la afya linaendelea Geneva

Kongamano la kimataifa la afya linaendelea Geneva

Leo ni kilele cha kuadhimisha ya siku ya pili inayojulikana kama kusanyiko la afya duniani WHA ambayo kilele chake kinatazamiwa kufikia May 24.

Ikiwa sehemu ya shamra shamra ya siku hii, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Margaret Chan akiwa na muasisi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates wanatazamiwa kuwa na mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Geneva, ambako wataelezea mambo mbalimbali.

Kwa upande mwingine WHO leo imeweka wazi bajeti yake kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 ambayo hata hivyo inakabiliwa na upungufu wa dola za kimarekani milioni 300.

Maazimio makubwa wakati wa maadhimisho ya mwaka huu yanaweka zingatio kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kukabiliana na kuibuka kwa mafua ya nguruwe, ufikiaji shabaya ya malengo ya maendeleo ya malenia na namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo kipindupindu.