Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kutuma wataalamu Japan

IAEA kutuma wataalamu Japan

Shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA linatarajiwa kutuma ujumbe wa wataalamu kwenda nchini Japan kufuatia maelewano kati ya IAEA na serikali ya Japan.

Ujumbe huo unaowajumuisha karibu wataalamu 20 wa kimataifa kutoka nchi kadha watazuru Japan kuanzia kati ya tarehe 24 Mei na Juni 2 mwaka huu. Wakiongozwa na Mike Weightman mkuu wa ukaguzi wa masuala ya kinyuklia kutoka Uingereza wataalamu hao watakitembelea kinu cha Fukushima Dai-ichi na sehemu zingine. George Njogopa ana ripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)