Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado kuna chuki dhidi ya mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia

Bado kuna chuki dhidi ya mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia

 

Ulimwengu unaendelea kukabiliwa na unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wasagaji , wasenge na watu walio na jinsi mbili au wanaobadili jinsia hali ambayo huenda ikaathitiri maisha yao au kuzua ghasia.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS Michel Sidibe anasema kuwa imegunduliwa kuwa wakati watu wanapobaguliwa kutokana na maisha yao ya kingono au jinsia huwa hawatafuti huduma za matibabu ya virusi vya ukimwi wanazohitaji hali inayochangia maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi na vifo vinayosababishwa na ugonjwa huo.

Sidibe amesema kuwa watu kama hao wanastahili kukubalika na kuvumiliwa na kutoa wito kwa serikali kuheshimu haki za binadamu na kuhakikisha kuwa wamepata huduma za matibabu. Naye mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay akizungumzia kuongezeka kwa chuki dhidi ya waliobadili jinsia amezitaka serikali kufanya kila juhudu kumaliza ubaguzi na chuki inayotokana na maisha ya kingono au jinsia za watu.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)