Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM akutana na maafisa wa serikali Tripoli

Mjumbe wa UM akutana na maafisa wa serikali Tripoli

Afisa wa ngazi za juu wa umoja wa mataifa amefanya ziara ya siku moja mjini Tripol nchini Libya na kufanya mazungumzo na  maafisa wa serikali ikiwa ni juhudi za kidiplomasia za kujaribu kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo.

Akiweka msukomo kwenye juhudi hizo mjumbe maalumu wa katibu mkuu nchini Libya Abdel Elah al-Khatib,amekutana na maafisa kadhaa wa serikali akiwemo waziri wa mambo ya nje, waziri mkuu pamoja katibu mkuu wa baraza kuu la Libya.

Viongozi hao wamejadiliana juu ya haja ya utekelezaji kikamilifu wa mazimio ya baraza la usalama ambayo yanaweka zingatio la kutolewa kwa misaada ya kisamaria hasa wakati huu ambapo hali ya usamala inazidi kuzorota.

Mwakilishi  huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa amepewa ushirikiano mkubwa.