WHO imezitaka serikali kuwalinda wahudumu wa afya katika vita:

16 Mei 2011

Shirika la afya duniani WHO limetoa wito kwa serikali kuhakikisha zinawalinda wahudumu wa afya na vituo vya afya katika wakati wa migogoro ili kuwawezesha kutoa huduma kwa wagonjwa na majeruhi.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kila mwaka wa afya mjini Geneva, mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Margaret Chan amesema amesikitishwa na mashambulizi ya karibuni dhidi ya wahudumu wa afya na vituo vya afya katika baadhi ya nchi zinazokabiliwa na machafuko ya kisiasa.

Dr Chan amesema ongezeko la idadi ya wanawake na watoto wanaoathirika katika vita inatia hofu na ametoa wito wa kukomesha ukatili wa kimapenzi dhidi ya wanawake na watoto.

(SAUTI YA MARGARET CHAN)

Mkutano huo wa kimataifa wa afya unawaleta pamoja nchi wanachama wa WHO ili kutathimini shughuli za shirika hilo na kuorodhesha vipaumbele vipya vya siku za usoni.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter