Mkutano wa UM waainisha mipango ya kuzikwamua nchi masikini kabisa duniani:Sefue

13 Mei 2011

Kwa Juma zima Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, naibu wake, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, wahisani , wawakilishi kutoka nchi tajiri , mashirika, jumuiya za kijamii, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na nchi masikini kabisa duniani walikusanyika mjini Istanbul Uturuki ili kutanabahi mbinu za kuzisaidia nchi hizo masikini kabisa kuondokana na hali hiyo iliyomea mizizi.

Mkutano huo umejadili kwa nini nini cha kufanya, hatua walizopiga tangu mkutano wa Brussels miaka 10 iliyopita na nini kifanyike katika miaka 10 ijayo kuhakikisha nchi hizo fukara kabisa 48 ninapungua japo kwa nusu katika miaka 10 ijayo. Nchi hizi zimeelezwa kughubikwa na umasikini wa kupindukia, uongozi mbomu na miundombinu duni.

Katika kuhitimisha mkutano huo ijumaa hii uliofungwa na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose- Migiro wadau wameafikiana kwamba sekta binafsi zitahitaji kuchukua jukumu kubwa hasa katika kuwekeza , lakini pia serikali hizo ambao nyingi ziko Afrika Kusini kwa jangwa la Sahara zina wajibu wa kutimiza kama anavyosema Cheick Sidi Diarra katibu anayehusika na nchi hizo maskini kwenye Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA CHEICK SIDI DIARRA)

Na mataifa tajiri yamekumbushwa kutekeleza ahadi zake za msaada kwa nchi masikini ambao ni sawa na asilimi 0.2 ya pato la taifa. Nchi Masikini zenyewe zinasema zilikwenda kwenye mkutano huo na malengo na zinaondoka na ahadi ambazo zinatumai zitawasaidia.

Kutathimini matarajio ya nchi maikini nimezungumza na balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Omben Sefue aliyehudhuria mkutano huo akisema nchi hizo masikini kwa kweli zimejitahidi

(MAHOJIANO NA BALOZI OMBEN Y. SEFUE) )

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter