UM wazungumzia hali ya mahabusu Ivory Coast

13 Mei 2011

Idara ya haki za binadamu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutoa huduma nchini Ivory coast UNOCI unasema kuwa hali ni ngumu kwa baadhi ya wale waliokamatwa pamoja na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo.

Wanasema kuwa kuna hali ngumu katika gereza la Bouna ambapo watu saba akiwa mwana wa kiume wa Gbagbo na rais wa kilichokuwa chama tawala ambao walikamatwa pamoja na bwana Gbagbo tarehe 11 mwezi Aprili mwaka huu.

Watetesi wa haki za binadamu kutoka UNOCI wameruhusiwa kuwatembea wanaozuiliwa kwenye mji wa Bouake ambapo pia hali inatia wasiwasi. Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu anasema kuwa wanajadili njia za kuwafikia wote waliokamatwa kutokana na ghasia za baaada ya uchaguzi.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter