Haki za binadamu Mashariki ya Kati bado zinakiukwa:Pillay

13 Mei 2011

Ofisi ya mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa bado kuna matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kuzima maandamano sehemu mbali mbali za mashariki ya kati.

Ofisi hiyo inasema kuwa kati ya watu 700 na 850 wameuawa na maelfu ya wengine kukamatwa. Kwa sasa inandaa ofisi hiyo inandaa kutuma ujumbe nchini Syria ambao utaongozwa na naibu mkuu wa tume ya haki za binadamu.

Pia kunaripotiwa ukiukaji zaidi wa haki za binadamu nchini Yemen hata kama madai yenyewe hayajathibitishwa huku ujumbe ukitarajiwa kutumia kwenda nchi hiyo mwezi Juni.

Nchi Bahrain ripoti zinasema kuwa mamia ya madaktari, wanaharakati wa kisiasa na watetesi wa haki za binadamu wamekamatwa. Pia kumekuwa na dhuluma na huenda wafungwa wamekufa baada ya kuteswa.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter