Suluhu ya Somalia ni kutekeleza muafaka wa kisiasa na kufanya uchaguzi:Mahiga

13 Mei 2011

Somalia ambayo kwa zaidi ya miongo miwili sasa haina serikali kuu inazidi kujikuta katika njia panda ya kisiasa kwa mgawanyiko kughubika uhusiano baina ya Rais wa serikali ya mpito na spika wa bunge.

Kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia balozi Agustine Mahiga tofauti hizo zinazidisha adha kwa mamilioni ya wasomali waliochoka vita na wenye kiu ya amani ya kudumu.

Bunge limejiongezea muda na serikali vivyo hivyo na wote hawataki kumaliza kipindi cha mpito kama ilivyopangwa awali hapo mwishoni mwa wezi Agosti hali ambayo inafanya kuwa vigumu kufikia malengo ya amani.

Sasa balozi Mahiga ameliomba baraza la usalama kwenye Nairobi Kenya siku chache zijazo kukutana na serikali ya mpito na kuifahamisha umuhimu wa kuzingatia matakwa ya mchakato wa amani.

Mahiga amekuwa hapa New York kuwasilisha ripoti yake kwa baraza la usalama na amemfahamisha mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa yaliyojiri

(MAHOJIANO NA BALOZI MAHIGA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter