Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili katika kilimo na viwanda utapunguza umasikini:UM

Ufadhili katika kilimo na viwanda utapunguza umasikini:UM

Uwekezaji katika kilimo na kujenga viwanda zaidi kwenye nchi maskini zaidi duniani vimetajwa kama njia ya kuboresha uchumi na kukabiliana na kupanda kwa viwango vya maisha katika nchi hizo.

Haya ni kulingana na katibu mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo la UNCTAD Supachai Panitchpakdi .

Akiongea na waandishi wa habari nchini Uturuki Supachai amesema kuwa kuimarika kwa uchumi kulikoshuhudiwa kati ya mwaka 2002 na 2007 kulichangia katika kuimarika kwa uchumi kwenye nchi maskini kwa asilimia saba kila mwaka.

Amesema kuwa kutotenga fedha kwa sekta ya kilimo kwenye nchi maskini kumesabaisha kukwama kwa chumi katika miaka ya hivi majuzi hata kama kilimo ndicho chanzo cha ajira kwenye nchi hizo.