Mkataba wa watoto utasaidia kuwalinda kwenye majanga:UNICEF

12 Mei 2011

Utafiti mmoja uliotolewa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na watoto UNICEF umeonyesha kuwa watoto wengi walioko kwenye maeneo yaliyokumbwa na majanga, moja ya vipaumbele wanavyopendelea ni kuwepo kwa majengo ya shule yenye usalama wakati wa dharura

Utafiti huo ambao umehusisha zaidi ya watoto 600 kutoka nchi 21 umeinisha masuala mengine kama elimu, ulinzi kwa watoto na kufikiwa na habari muhimu ni maeneo mengine ya muhimu ambayo yanapaswa kuzingatiwa ili kupunguza msongo wa athari unaojitokeza wakati wa majanga.

Utafiti huo sasa umepiga hatua kubwa ambapo unataka kuwepo kwa mkataba maalumu ambao utajadiliwa na nchi wanachama kwenye mkutano huko Geneva kabla ya nchi hizo kuambwa kuridhia mkataba huo unaopendekezwa hatua za kuchukuliwa ili kuwalinda watoto wakati wa majanga.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter