Michezo itumike kuharakisha maendeleo duniani:Ban

12 Mei 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitolea mwito nchi zote ulimwenguni kuhakikisha kwamba zinaowanisha mipango yao na shughuli za kimichezo kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo.

Akizungumza mjini Geneva kwenye kongamano la pili linalojadilia masuala ya michezo, amani na maendeleo, Ban amesema kuwa nchi nyingi dunia zinapaswa kuchukua hatua hiyo kwani michezo inanafasi kubwa ya kuchangia kwenye  ufikiaji wa shabaya ya malengo ya maendeleo ya mellenia.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa daima unadhamini na kutambua umuhimu wa michezo na ndiyo maana mara nyingi hutumia michezo ili kuzisaidia jamii nyingi duniani.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter