Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu huru wa haki za binadamu kuzuri Burundi

Mtaalamu huru wa haki za binadamu kuzuri Burundi

Mtalaamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Burundi Fatsah Ouguergouz atazuru nchini humo kuanzia Mai 16 hadi 20 kukusanya taarifa kutoka pande zote kuhusu hali ya haki za binadamu. Mtaalamu huyo atafuatilia hususan madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu za kuishi, uhuru wa kujieleza na kukusanyika, kuheshimiwa kwa utu wa mtu na pia hatua zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na ukwepaji wa sheria.

Pia mtaalamu huyo atatathimini juhudi za serikali kuanzisha tume huru ya haki za binadamu ambayo iliundwa kisheria Januari 5 mwaka huu. Mbali ya kukutana na viongozi mbalimbali mjini Bujumbura atazuru pia magereza mjini Ngozi na kuzungumza na wawakilishi wa jumuiya za kiraia na viongozi wa jimbo. Na atatoa taarifa yake kuhusu hali ya haki za binadamu Burundi kwenye mkutano ujao wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva.