Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa makazi unatishia ndege wanaohama kimataifa:UNEP

Upungufu wa makazi unatishia ndege wanaohama kimataifa:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limesema upungufu wa makazi unatoa tishio la kimataifa kwa ndege wanaohama. UNEP inasema ndege hao katika maisha yao husafiri maelfu ya kilometa wakivuka mipaka toka nchi moja na nyingine na kupitia mifumo mbalimbali ya maisha.

Kila mwaka ndege wanaohama wanakadiriwa kuwa bilioni 50 wakiwakilisha asilimia 19 ya aina 10,000 ya ndege duniani, na kila mwaka makazi ya asili ya ndege hao ama yanapungua au kutoweka kabisa. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)