Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubakaji DRC umefurutu ada kila saa wanawake 48 wanabakwa:UM

Ubakaji DRC umefurutu ada kila saa wanawake 48 wanabakwa:UM

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ukatili wa kimapenzi Margot Wallstrom akiongelea ripoti ya utafiti kuhusu ubakaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao umeelezewa kufutu ada kwa wanawake 48 kubakwa kila saa, amesema tafiti kama hizo ni muhimu.

Utafiti huo uliochapishwa leo na jarida la Marekani la afya ya jamii AJPH, Bi Wallstrom amesema unatoa mwangaza wa nani na wapi vitendo hivyo vya kikatili vinafanyika.

Ameongeza kuwa wakati ofisi yake ikijikita kushughulikia ukatili wa kimapenzi katika maeneo ya vita ambako mara nyingi ubakaji hutumika kama silaha ya vita’ utafiti wa AJPH umebaini kwamba wanawake takribani milioni 1.8 wa kati ya miaka 15 na 49 wamearifu kubakwa, huku wengine milioni 3 wamefanyiwa ukatili wa kimapenzi na wapenzi wao, na kufanya wanawake wane kubakwa kila dakika tano.