Skip to main content

Somalia inakabiliwa na mtafaruku wa kisiasa:Mahiga

Somalia inakabiliwa na mtafaruku wa kisiasa:Mahiga

Kuna khadhia ya kisiasa Moghadishu ambako Rais na spika wa bunge hawana mawasiliano, amesema mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga.

Mahiga amelimia leo baraza la usalama kwamba nchi hiyo ambayo haina serikali kuu tangu mwaka 1990, serikali ya mpito inapaswa kumaliza muda wake mwezi Agosti ambapo serikali inapaswa kufanya uchaguzi.

Ameongeza kuwa kutokana na ukweli kwamba bunge limejiongezea muda wake na serikali kuahirisha uchaguzi kwa mwaka mmoja, ni hali iliyochagia kuzorotesha zaidi uhusiano baina ya serikali na bunge taasisi mbili muhimu katika nchi hiyo iliyoghubikwa na vita.

Mahiga amesema hivyo kuna haja ya kupata muafaka haraka wa lini na jinsi gani uchaguzi utafanyika na kumaliza mvutano baina ya taasisi hizo mbili muhimu.