Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi na ukosefu wa usalama Syria watia hofu:UM

Mashambulizi na ukosefu wa usalama Syria watia hofu:UM

Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na usamaria mwema Bi Valerie Amos ameelezea kusikitishwa kwake na namna ambavyo wananchi wa Syria wanavyobinywa ili kufikiwa na huduma za dharura.

Amesema kuwa ripoti nyingi zinaonyesha kwamba pamoja na ugumu wa kupatiwa huduma za usamaria mwema, lakini waandamanaji wengi wameuliwa wakati wanapojaribu kujitokeza kwenye mikusanyiko ya watu.

Matukio hayo yamearifiwa kujitokeza kwa wingi katika miji madhaa ikiwemo miji ya  Deraa,Latakia, Jablah, Baniyas na  Douma.

Kabla ya kutoa matamshi hayo Bi Amos alizungumza kwenye baraza la usalama akiweka msisitizo haja ya kulindwa kwa raia kwenye maeneo yenye mizozo.