Vikosi vya UM vyashambuliwa Abyei Sudan

Vikosi vya UM vyashambuliwa Abyei Sudan

Wafanyakazi kadhaa wa umoja wa mataifa wanaofanya kazi katika vikosi vya kulinda amani nchini Sudan wamejeruhi baada ya msafara wao wa doria kuvamiwa na makundi ya watu katika jimbo linaloshuhudia machafuko la Abyei.

Ripoti zinasema kuwa waliojeruhiwa na askari wanne wakati walipovamiwa katika kijiji cha Goli eneo lililopo maili 15 kutoka Abyei. Maafisa wa umoja wa mataifa wamelani shambulizi hilo na kusema kuwa ni kitendo cha kichokozi ambacho ni chakupuuzi.

Jimbo la Abyei kwa hivi sasa linashuhudia hali ya machafuko ya hapa na pale na kunaarifiwa kuwa kumekuwa na umwagikaji mkubwa wa damu.