Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta binafsi ni nguzo ya kuinua uchumi katika nchi masikini

Sekta binafsi ni nguzo ya kuinua uchumi katika nchi masikini

Sekta za kibinafsi zina wajibu mkubwa kusaidia kuimarisha maendeleo kwenye nchi maskini zaidi nyingi zikiwa barani Afrika.

Hii ni kulingana na mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uongozi bora la Global Compact George Kell. Nchi 48 zinazotambuliwa kama nchi maskini zaidi huwa zikikabiliwa na umaskini , uwekezaji kidogo na miundo mbinu mbaya.

Kell anasema kufanikiwa kwa maendeleo kutahitaji uwekezaji wa kibinafsi akiongeza kuwa ili kufanikiwa ni lazima nchi iwe na uhusiano na sehemu zingine za dunia utakaochangia uwekezaji wa kigeni suala ambalo huleta teknolojia mpya na kupatikana kwa masoko.