Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zimetakiwa kufikiria masuala ya jinsia katika sera za biashara

Nchi zimetakiwa kufikiria masuala ya jinsia katika sera za biashara

Ripoti ya Umoja wa mataifa iliyotolewa leo imesema lengo la upanuaji wa biashara katika taifa la Bhutan na kudumisha tija ya taifa hilo la Asia lazima lishirikishe mikakati ya elimu kwa wanawake na kuinua uwezo wao katika jamii na masuala ya kiuchumi.

Ripoti hiyo isemayo nani ananufaika na biashara huria Bhutan, kwa mtazamo wa jinsia, iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD ni moja ya tathimini ya athari za jinsia katika maendeleo ya nchi hususani masikini sana.

Ripoti hiyo itatoa fursa ya mjadala leo kwenye mkutano wan chi masikini mjini Istanbul Uturuki watakapokuwa wakiangalia suala la wanawake na biashara .

UNCTAD inasema mchakato wowote wa maendeleo unaoacha kundi kubwa la watu nyuma haukubaliki na badala ya kuimarisha utakuwa unadumaza maendeleo.